Sura Al-Haqqah

Aya

52

Mahali iliteremshwa

Makka

SURAT AL-H'AAQQAH 

(Imeteremka Makka) 

Sura hii tukufu inaeleza hali za Kiyama, na imetaja yaliyo wasibu watu wa mataifa yaliyo tangulia, ya kuteketezwa, na kuchukuliwa kwa nguvu na shida walipo kadhibisha. Na imetaja namna litavyo pulizwa baragumu na mageuzi na kuondoka yatakayo zisibu ardhi na milima na mbingu. Na yatakayo tokea baada ya hayo ya kuletwa watu kwa ajili ya hisabu, na kubashiriwa watu wa mkono wa kulia kwa malipo ya ukarimu na neema za daima watakazo zipata, na maonyo ya watu wa kushoto na adhabu chungu. Tena Sura ikakhitimisha kwa kutaja ukweli wa Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w. katika Ujumbe alio ufikisha, na ukweli wa Qur'ani ambao ndio ni Haki iliyo yakini.