Sura Al-Lahab

Aya

5

Mahali iliteremshwa

Makka

SURAT AL-MASAD 

(Imeteremka Makka)

Sura imeanza kwa kutoa khabari kuhiliki kwa Abu Lahab, adui wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kuwa hapana kitu cha kumfaa, mali wala cheo au vyenginevyo, na inamuahidi kuwa Akhera ataingia Motoni na ataungua humo, pamoja na mkewe ataye kuwa naye. Na yeye amekhusishwa kwa adhabu ya kufungwa kamba katika shingo yake ya kumvutia mpaka kwenye Moto katika kuzidi kumuadhibu kwa sababu ya maudhi yake aliyo kuwa akimfanyia Mtume na maovu aliyo kuwa akiyafanya kupinga Wito.