Sura An-Naziat

Aya

46

Mahali iliteremshwa

Makka

SURAT ANNAZIA'AT 

(Imeteremka Makka)

Imeanza Sura hii kwa kiapo juu ya kumkinika kufufuliwa na kutokea kwake, na ikafuatia hayo hadithi ya Musa na Firauni kumliwaza Mtume s.a. w., na ikataja khabari za binadamu na juhudi zake na ikadhihirisha yanayo wangojea majabari, na yanayo za binaadamu na wangojea makhaini. Na Sura ikakhitimisha kwa kuuliza kwao washirikina lini itakuwa hiyo Saa ya Kiyama, na ikabainisha kwamba kazi ya Mtume ni kuwaonya wenye kukiogopa Kiyama, sio kujua wakati wake.