Sura At-Tariq

Aya

17

Mahali iliteremshwa

Makka

SURAT ATT'AARIQ 

(Imeteremka Makka)

Sura hii imeanzia kwa kiapo cha kuashiria dalili za kudra ya Mwenyezi Mungu, na inatilia mkazo kuwa kila nafsi ina mlinzi wake na muangalizi, na inamtaka mtu ajifikirie kuumbwa kwake, na ya kwamba yeye kaumbwa na maji yenye kutoka kwa kasi, ili ipatikane hoja kwamba Mwenye kuumba hivi ni Mweza wa kumrejeza tena  na baada ya kufa kwake.Tena ikaapa mara ya pili kwamba Qur'ani ni kauli ya kufafanua wala si maneno ya maskhara. Na juu ya kuwa hivyo makafiri bila ya shaka wameshughulika kuikanya na kuipangia njama. Na Mwenyezi Mungu arezirudi njama zao kwa njama kali kuliko zao. Kisha Sura imekhitimisha kwa kutaka wapewe muhula makafiri.