Aya
12
Mahali iliteremshwa
Madina
SURAT ATT'ALAAQ
(Imeteremka Madina)
Sura hii inaeleza baadhi ya hukumu za talaka, na eda, na namna zake, na hukumu zake tangu kubaki mwenye eda katika nyumba aliyo pewa talaka ndani yake, na waajibu wa kumtazama kwa matumizi, na maskani. Na kati ya hukumu hizi, kama ilivyo mwendo wa Qur'ani, ipo ahadi kwa mwenye kufuata amri za Mwenyezi Mungu, na onyo kwa mwenye kukiuka mipaka yake.
Kisha Sura imeashiria malipo ya wenye kutakabari wakakataa kutimiza amri za Mwenyezi Mungu na Watume wake. Na ikakhitimisha Sura kwa kuwahimiza Waumini wamche Mwenyezi Mungu, na kuwakumbusha neema za kuwapelekea Mtume anaye wasomea Aya za Mwenyezi Mungu, ili awatoe kwenye giza wende kwenye mwangaza, na kwa uweza wake Mwenyezi Mungu kuziumba mbingu saba, na katika ardhi mfano Wa hizo.