Aya
30
Mahali iliteremshwa
Makka
SURAT ASSAJDAH
(Imeteremka Makka)
sura hii iliteremka baada ya Surat Al Muuminun. Nayo imekusanya mazungumzo juu ya kuteremshwa Kitabu, na umuhimu wa Mtume s.a.w. na kuumbwa mbingu na ardhi, na shani yake Mtukufu katika kupanga, na kumlea na kumuendeleza kumuumba mwanaadamu, na maneno ya wenye kukanya kufufuliwa na jawabu ya kuwajibu, na hali ya wakosefu Siku ya hisabu, na msimamo wa Waumini wakati zinapo tajwa Aya, na kubainisha malipo ya Waumini na waovu, na kuteremshiwa Musa a.s. Taurati, na vipi alivyo waamili Mwenyezi Mungu Wana wa Israili, na kuwaelekeza makafiri wa Makka wazingatie walivyo angamia walio watangulia, na kuwataka watazame kwa macho yao ili waamini kufufuliwa. Na Sura imetaja vipi hao makafiri walivyo ifanyia kejeli siku ya ushindi, na jawabu walio pewa.
Na lengo muhimu la Sura hi ni kuelekeza nadhari kwenye Ishara za ulimwengu ulivyo umbwa, na mazungumzo juu ya kufufuliwa, na jawabu za kuwarudi hao wanao kanya kufufuliwa, na kuwaelekeza makafiri wazingatie maangamizo yaliyo wasibu walio watangulia.