Sura Al-Mujadilah

Aya

22

Mahali iliteremshwa

Madina

SURAT AL-MUJAADALAH 

(Imeteremka Madina)

Sura imeanza kwa kueleza khabari za mwanamke anaye tengwa na mumewe, na ikafuatia kubainisha hukumu za kutengana. Na Mwenyezi Mungu katika sura hii katika zaidi ya Aya moja amewatia makosani wanao ifanyia uadui Dini yake, na amewahadharisha na kunong'ona nong'ona kwa ajili ya madhambi na uadui. Na amewaongoza Waumini juu ya adabu za kunong'ona baina yao kwa wao, na baina yao na Mtume s.a.w. Kama vile vile alivyo watia makosani wanaafiki kwa kushirikiana na makafiri. na akawaeleza kuwa hao ni kundi la Shetani lenye kuingia khasarani.

Na Sura ikakhitimisha kwa kueleza kwa jumla yaliyo ya waajibu juu ya Waumini ya kupendelea kumridhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuliko wengine wasio kuwa wao, hata wangeli kuwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Na akawasifu Waumini hao kuwa ni Hizbu-Llahi, Kundi la Mwenyezi Mungu, lenye kufanikiwa.