Sura Al-Muzzammil

Aya

20

Mahali iliteremshwa

Makka

SURAT AL-MUZZAMMIL 

(Imeteremka Makka)

Katika Sura hii Mwenyezi Mungu amemuamrisha Mtume wake asimame sehemu kubwa ya usiku kwa ajili ya Sala na kusoma Qur'ani kwa utulivu. Akawa anasimama yeye na kikundi cha wale walio kuwa pamoja naye Kisha Mwenvezi Mungu aliwapunguzia na akawaamrisha Sala, na Zaka, na Sadaka na Kuomba maghfira.

Na miongoni ya hayo akamuamrisha avumilie kwa wayasemayo wale wanao kadhibisha, na awaachilie iwapate adhabu aliyo waahidi Mwenyezi Mungu; na Yeye amewaonya makafiri kwa mfano wa adhabu iliyo mshukia Firauni na walio kuwa pamoja naye, walipo muasi Mtume wa Mola wao Mlezi, na akawakhofisha kwa vitisho vya Kiyama.