Sura Al-Bayyinah

Aya

8

Mahali iliteremshwa

Madina

SURAT AL-BAYYINAH 

(Imeteremka Madina)

 Watu wa Kitabu, yaaani Mayahudi na Wakristo, wamejua kutokana na Vitabu vyao, na washirikina wa Makka wakajua kutokana nao sifa za Nabii wa zama za mwisho. Na yalikuwa yanatakikana kutokana na hayo ni kuwa wamuamini huyo Nabii pind akiteuliwa. Lakini alipo teuliwa miongoni mwao Mtume wa Mwenyezi Mungu mwenye kuungwa mkono na Qur'ani, walikhitalifiana na wakaacha ahadi yao. Na vitendo vya Watu wa Kitabu katika hayo vilikuwa viovu zaidi kuliko vya washirikina Na hukumu ya watu hawa wote Akhera ni kukaa milele katika Moto. Na Waumini, watu wa vyeo vya juu kwa fadhila, ndio bora wa viumbe. Malipo yao ni kukaa milele Peponi, na kuridhika kwa kuyapata wayatakayo na kupewa wanayo yapenda. Hii ndiyo neema ya mwenye kumkhofu Mola wake Mlezi.