Aya
20
Mahali iliteremshwa
Makka
SURAT AL-BALAD
(Imeteremka Makka)
Mwenyezi Mungu anaapa kwa mji mtakatifu wa Makka, mji wa kuzaliwa Muhammad s.a.w. na ndipo alipo kulia na akapapenda, na pia anaapa kwa mzazi na anacho kizaa kwani kwa hao ndio jinsi inahifadhika na maamrisho yanabakia, na ya kwamba mtu ameumbwa kwa mashaka na shida na taabu. Tena anabainisha kwamba mtu anadanganyika kwa kudhani kuwa uweza wake haushindiki, na kwamba yeye ana mali mengi anayo yatumia kuridhisha matamanio yake na pumbao lake. Kisha Subhanahu akazitaja neema alizo mneemesha mwanaadamu na kumsahilishia njia za uwongofu na za kupitia milimani, ili awe katika watu wa Peponi, watu wa mkono wa kulia, na aikimbie njia ya kumpelekea kuwa katika watu wa kushoto ambako itawatumbukiza Motoni na kufungiwa milango.