Sura Al-Qadr

Aya

5

Mahali iliteremshwa

Makka

SURAT AL-QADR  

(Imeteremka Makka)

Katika Sura hii inasifiwa shani ya Qur’ani na shani ya Usiku ilipo teremshwa Qur'ani na inaelezwa kwamba usiku huo mmoja ni bora kuliko miezi elfu, na kwamba hakika Malaika na Jibrili huteremka usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa ajili ya kila amri, kwa kusalimika na kila maudhi na uovu mpaka kuchomoza alfajiri yake.