Aya
8
Mahali iliteremshwa
Makka
SURAT ASH-SHARH
(Imeteremka Makka)
Inathibitisha Sura hii kwamba Mwenyezi Mungu ameukunjua moyo wa Nabii wake, na akaufanya ndipo pahala pa kuteremkia siri na ilimu, na akaondoa matatizo yaliyo kuwa Inathibitisha Sura hii kwamba Mwenyezi Mungu ameukunjua moyo wa Nabii wake, na yakimthakilisha mgongo wake. nayo ni katika mizigo ya kazi ya Da'wa yaani Wito. Na akalikutanisha jina lake Mwenyezi Mungu na jina lake Mtume katika asli ya Imani mepesi na mazito, dhiki na faraji, na zikamtaka Mtume kila anapo pata nafasi kutokana na alama za Dini. Kisha Aya hizi zikataja sunna ya Mwenyezi Mungu ya kuambatisha , na kutenda kheri, atende kheri nyengine, na afanye lengo lake ni Mola wake Mlezi, kwani Yeye ni Muweza wa kumsaidia.