Sura Al-Asr

Aya

3

Mahali iliteremshwa

Makka

SURAT AL-A'S'R 

(Imeteremka Makka)

Katika Sura hii anaapa Subhanahu kwa Zama, kwa zilivyo kusanya chungu ya ajabu na mazingatio yenye kujuulisha uweza Wa Mwenyezi Mungu na hikima yake, ya kwamba mtu haachi kuwa na upungufu katika vitendo vyake na hali zake ila Waumini wanao tenda mema, na wakausiana kushika Haki Na hiyo ndiyo kheri yote. Na wakausiana kusubiri na kuvumilia juu ya walio amrishwa na walio katazwa.