Sura At-Tahrym

Aya

12

Mahali iliteremshwa

Madina

SURAT ATTAH'RIIM 

(Imeteremka Madina) 

Sura hi inaashiria jambo ambalo lilimuudhi Nabii s.a.w. katika baadhi ya wake zake akajizuilia na baadhi ya mambo ambayo nafsi huyapenda na Mwenyezi Mungu amehalalisha. Na inawahadharisha wake zake na matokeo ya waliyo yatenda. Kishe Sura ikaingia kuwaamrisha Waumini waiikinge nafsi zao na ahali zao na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Na ikabainisha kwamba haukubalii udhuru wa makafiri Siku ya Kiyama. Na inawataka Waumini watubu kweli kweli, na Mtume s.a.w. ende kupambana kwa Jihadi na makafiri na wanaafiki, na awe mgumu kwao. Na inakhitimisha kwa kupiga mifano kwamba wema wa waume hautazuia adhabu isiwafikie wake zao wakiwa wao wamepotoka, na kwamba uharibifu wa waume hauwadhuru wake zao ikiwa hao wake wamesimama sawa sawa. Kwani kila nafsi ina dhamana kwa vitendo vyake mwenyewe.