Sura Ash-Shuaraa

Aya

227

Mahali iliteremshwa

Makka

SURAT ASH-SHUA'RAA 

(Imeteremka Makka)

Sura hii imeanzia kwa kuisifu Qur'ani yenyewe, ikaingia kuwaonya makafiri kwa uweza wa Mwenyezi Mungu kuwateremshia adhabu juu yao, na kumliwaza Nabii s.a.w. kwa anayo yapata ya kukanushwa na watu wake, kwa kutajiwa yalio wapata Mitume wa kabla yake ya kukadhibishwa na kaumu zao. Ikasimulia mkutano wa Musa na Harun walipo kutana na Firauni, na alivyo wakadhibisha yeye. Kisha Subhanahu akataja kisa cha Ibrahim. baba wa Manabii, na khabari za Nuhu pamoja na kaumu yake, na mambo ya A'adi, na Saleh pamoja na Thamud. Kisha ikaelezea Sura wito wa Luti na kisa cha Shuaib na watu wa Vichakani (Al-Aykat). 

Na mwenye kuzingatia visa vya hawa Manabii saba ataona asili ya wito wao ni mmoja, Na njia ya makafiri katika kupinga ujumbe wao ni moja. Kama ilivyo anzia Sura basi ilikhitimishia mazumgumzo kwa kuvunja wazo la kuwa Mtume ni mtunga mashairi, na kuwa Qur'ani ni mashairi.